Skip to main content

MWENENDO MWEMA, NA TABIA NJEMA KWA KUHESHIMU HEKALU LA ROHO MTAKATIFU:

Kwa kuwa miili yetu ilifanywa kuwa mahali ambapo Roho Mtakatifu (Yesu Kristo) ataketi na kukaa nasi katika kutuelekeza namna ya kuenenda katika uhalisia wa Neno,
Tusome maandiko;

1 Wakorintho 6:20

19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
Kama mkristo halisi unatakiwa utambue ya kuwa wewe ni hekalu la Roho mtakatifu maana tulikwisha kukombolewa na sisi si Mali yetu wenyewe yaani hatuwezi kujimiliki kwasababu yupo aliye mkuu kuliko sisi ambaye ndie anayetumiliki sisi (Bwana Yesu Kristo), na dhahiri ya kwamba tunajua ya kuwa Roho mtakatifu hafungamani na dhambi sasa Ikiwa unajiita mkristo alafu umeshindwa kufanya mwili wako kuwa hekalu la Roho mtakatifu kwa kujitunza kulingana na Neno, na kuepuka maovu yatokanayo na miili hii, bila shaka shetani ataufanya huo mwili utumike kama anavyotaka yeye maana ukisha mkataa Roho mtakatifu shetani huchukua nafasi na ndipo mtu anajikuta akizama katika dhambi kila siku, yaani atatubu lakini atarudi tena kwa kuwa tayari yupo katika milki ya shetani, sasa tuone jinsi Mkristo halisi anavyotakiwa kuenenda, kwanza anatakiwa awe tayari kuuandaa mwili wake kuwa sehemu ambayo Roho mtakatifu atakaa kwa kujitakasa na kuepuka dhambi zitokanazo na matamanio ya mwili, Ikiwa unaenda kanisani hata kwa wiki Mara tano lakini bado hujauweka mwili wako kuwa sehemu ya Roho mtakatifu yani ujue ile ibada iliyo ya muhimu tayari umekwisha ikosa,
Tusome maandiko,
Warumi 12:1
Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
Umeona ibada iliyo ya maana? Sio kusema Yesu anaangalia Moyo haangali nnje, huo ni upotofu wa hali ya juu maana Mkristo halisi hudhiirika katika Maisha yake halisi, sasa kwa hilo lililo wapoteza wengi usipo kuwa nalo makini litakupeleka kwenye milki ya muovu ibilisi.
Waumini wengi wakati huu wanasema wameokoka lakini hawafuati Neno, je huoni yakuwa wanakiri dhambi ya uongo mbele ya hayo wanao washuhudia waokovu wao?
Utakuta wanawake kanisani wanajipamba kwa vipodozi vya kila aina ili kufanya miili yao kuonekana yapendeza mbele za watu kumbe Mbele za Mungu ni chukizo, kupaka midomo rangi huku unasema umeokoka ni kujidanganya tuu na kujipa moyo, maana ile nguvu ya upotevu tayari I juu yako, na wengi wao wakisuka nywele zao kuona kwamba wapo sahihi kumbe wanalipinga Neno, sasa hebu tuone maandiko yanavyosema juu ya wanawake wanavyotakiwa kuiheahimu miili yao,

1 Timotheo 2:9-10

9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.
Umeona? Watu waamecha kupamba miili yao kama hekalu  la Roho mtakatifu na matokeo yake wamejipamba kama namna ya ulimwengu ilivyo kuonyesha wanakiri kuwa wamempokea Yesu lakini kumbe wapo kwenye Milki ya Shetani, hapo ndipo utaona ukisha jiweka kwa namna ya kidunia lazimazile njia za kutenda dhambi zitakujia kwa kila Namna na hatimaye utaangukia mikononi wa shetani, maana siku hizi watu wamefanya hadi miziki ya kidunia kuwa sehemu za maisha yao, hadi  kudiriki kusema huwa zinaondoa mawazo kumbe tayari ibilisi amewawekea hali ya utegemezi ndani ya miziki ya kidunia ili wamsahau Yesu Kristo aliye mfariji wa ajabu, sasa  tujiulize kwaini watu hukataa Neno? Kwa nini hawataki kuenenda kama Wakristo halisi ? Jibu ni kwamba shetani hufanya kazi kwa njia amambazo mtu ataona ni za kawaida lakini kumbe anajiandaa kuanguka katika shimo la upotevu.
Na kwa upande wa wanaume, wamepoteza ule uhalisia na nguvu ambayo ilikuwako nyuma yao ndani ya kanisa, kwa kuenenda tuu kama wale wa ulimwengu wanavyoenenda ,kama ilipokwisha kuandika pale mwanzo kuwa kumuamini Yesu Kristo kuwa ni Bwana NA Mwaokozi wa maisha yetu ni kwamba lazima uwe umeamini Neno kwanza linavyoagiza wewe kama Mkristo kuenenda sasa ,siku hizi wanaume has a vijana makanisani ndio wamepotea kanisa kwa kukiri wameokoka huku angali hawaliamini Neno linavyo waonya kuanzia uvaajia hadi  mwenendo wao, kwa kuwa wamepotea kanisa kwa kuzitizamia namna za kidunia kama vile ndio Biblia imeagiza kumbe si Kweli ni wao kuzifuata njia za kidunia tena za maovu ibilisi, maana kwa ujio wa namna mbali mambali za kunyoa nywele siku hizi vijana wanaosema wameokoka ndio wanaongoza kwa kunyoa hivyo (denge) bila ya wao kujua ni chapa ya shetani wanajivika katika miili yao, na wengine kuacha manywele marefu kuona kama ni fashion kumbe ni kulingana na Neno, tusome maandiko,

1 Wakorintho 11:14

Je! Hayo maumbile yenyewe hayawafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake?

Je  Unalifurahia jambo hilo? Kusema umeokoka kumbe unajivika aibu yako kila uendako, sasa kwa kuwa ukilikataa Neno (Kweli) nguvu ya upotevu itaachiliwa kwako na utaendelea kuuammini uongo yaan utaendelea kuona wewe kuwa na nywele ndefu haiduru kitu wala hakuna shida kumbe ile hukumu ya kuikataa Kweli tayari utakuwa juu yako na ile chapa ya shetani tayari utakuwa nayo.
Tusome maandiko,

 Mambo ya Walawi 19:27

Msinyoe denge pembe za vichwani, wala msiharibu pembe za ndevu zenu.
Tusome pia,

Yeremia 49:32

Na ngamia zao watakuwa mateka, na wingi wa makundi yao utakuwa nyara; nami nitawatawanya hata pepo zote watu wale wanyoao denge; nami nitaleta msiba wao toka pande zao zote, asema Bwana.
Aina hii ya unyoaji ilikwisha kufanyika alama juu ya wale wamchukizao Mungu, sasa kunyoa denge ni kunyo nywele upande mmoja na kuacha zingine, sasa huu ni uhuni kabisa lakini wapo vijana makanisani wanajiita waliookoka lakini sana alama hizi vichwani mwao, Ni Mungu wa namna gani anayedhaniwa kuwa ana watu wa namna hii??? La hasha hakuna Bali hao ni wa shetani sio wa yule Mungu aliye HAI, maana amewek njia ambazo watu wake wataenenda wakimtukuza sasa ukienda kinyume na hapo wewe si wake ila tuu unajisemea kukuridhisha kinywa na moyo wako, waokovu huendana na kubadilishwa kila namna kuanzia muonekano wako, kunena kwako na njia zote za maisha yako halisi.
Sasa kaa  utafakari, juu ya hili, Ikiwa wewe ni mmoja kati ya watu wa kikundi Fulani chenye sheria na kanuni zake, na kila anayejiunga na kutambulika ni yule atakaye zifuata zile sheria zilizo wekwa tofauti na hapo utakuwa sio miongoni mwa watu hao, Wakristo halisi ambao Mienendo yao imeelezwa katika Biblia Takatifu ni wale ambao maisha yao yanaongozwa na Neno , tofauti na hao wanao ongozwa na Neno (Yesu Kristo)  hao ni wa milki nyingine ambayo ni ya muovu ibilisi.
Ndugu, chagua sasa uamuzi ni wako,
 Maisha yako yaongozwe na Neno au yaongozwe na ulimwengu na uelekee katika shimo la upotevu.


BWANA YESU KRISTO AKUBARIKI 









Comments

Popular posts from this blog

NJIA YA KWELI YA WOKOVU KULINGANA NA BIBLIA

Ikiwa ipo njia ya kweli ya wokovu, bila shaka na kwa uhakika njia ya uongo nayo itakuwepo maana Neno ambalo limeandikwa kwenye Biblia takatifu limeonyesha juu ya uongo na ukweli,  na kuwepo kwa roho ya uongo juu ya Ukristo halisi:,       1 Yohana 4:1-6   Wapenzi , msiamini kila roho kwamba zimetokana na Mungu Bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwasababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu na hii ndiyo Roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani. Ninyi watoto wadogo, mnatokana na Mungu ninyi mmewashinda, kwasababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia. Hao ni wa dunia; kwahiyo hunena ya dunia na dunia huwasikia; Sisi twatokana na Mungu yeye amjuaye Mungu atusikia; Yeye asiyetokana na Mungu hatusikii. Katika hili ...

KANISA LA MUNGU WA KWELI ALIYE HAI, NA NGUZO YA MSINGI WA KWELI

Biblia Takatifu kamwe haijawahi kukosea katika kutuelekeza njia sahihi ya kuishi na kuenenda katika ibada zetu kama Wakristo halisi, yapo Makanisa mengi sana duniani tena katika nyakati hizi za mwisho na mengine yalikuwako tokea miaka Mingi sana iliyopita, naYanaenenda katika njia tofauti tofauti, hili likimpinga yule, lingine likijaribu kujiinua juu ya lingine lakini yote hayo ni yamesababishwa na kanuni za imani zilizo wekwa ndani ya Makanisa hayo yaani Madhehebu , maana katika Madhehebu zipo kanuni ambazo zinakuwepo kuendesha dhehebu husika , na pia kanuni za imani juu ya dhehebu moja na jingine huwa zinatofautiana sasa tujiulize Kama wote tunanajiita wakristo na tunamuamini Bwana Yesu Kristo kuwa ndiye Neno iweje Leo watofautiane katika hilo Neno? tuangalie mfano halisi dhehebu la Lutheran wanabatiza watoto wadogo, na wanaruhusu wanawake kuhubiri,ukiangalia Roman catholic pia wanabatiza watoto wadogo lakini hawarusu wanawake kuhubiri , Pentekoste nao wanabatiza watu wazima kwa maji...