Ikiwa ipo njia ya kweli ya wokovu, bila shaka na kwa uhakika njia ya uongo nayo itakuwepo maana Neno ambalo limeandikwa kwenye Biblia takatifu limeonyesha juu ya uongo na ukweli, na kuwepo kwa roho ya uongo juu ya Ukristo halisi:,
1 Yohana 4:1-6
Wapenzi , msiamini kila roho kwamba zimetokana na Mungu Bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwasababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu na hii ndiyo Roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani. Ninyi watoto wadogo, mnatokana na Mungu ninyi mmewashinda, kwasababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia. Hao ni wa dunia; kwahiyo hunena ya dunia na dunia huwasikia; Sisi twatokana na Mungu yeye amjuaye Mungu atusikia; Yeye asiyetokana na Mungu hatusikii. Katika hili twamjua Roho wa kweli na roho ya upotevu.Mathayo 24:24-28
Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu wapate kuwapoteza ,kama yamkini hata walio wateule. Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. Basi wakiwaambia, yuko jangwani msitoke, msitoke yumo nyumbani, msisadiki kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyo kuja kwake Mwana wa adamu. Kwa kuwa po pote ulipo mzoga, ndipo watakapo kusanyika tai.
Tumeona baadhi ya Maandiko yaliyodhihirisha kuwepo kwa uongo na ukweli katika Ukristo, haya yote yametokana ile shauku ya kuabudiwa ambayo ibilisi alikuwa nayo, kabla ya kutupwa duniani na kama jina lake lilivyo "baba wa uongo" ndivyo alivyoleta uongo ndani ya Ukristo halisi ili wale waenendao katika ule uongo basi wawe wametimiza ile shauku yake ya kuabudiwa maana kukaa katika uongo ni kuwa upande wa Upotevu.
Katika Ukristo yapo mambo muhimu ambayo yatatimiza ukamilifu wa mwanadamu kuwa katika njia ile ambayo Bwana Yesu Kristo aliitazamia kanisa lake la kweli kuenenda, na sio kutokana na mawazo ya mtu binafsi bali katika Yeye pekee ambaye ni Neno, nalo tunalipata katika Biblia Takatifu.
Tutazame mambo hayo kama ifuatavyo,
1. KUMWAMINI NA KUMPOKEA YESU KRISTO KUWA BWANA NA MWOKOZI WAKO
Imani huja kwa kusikia, kwa kawaida mwanadamu huamini jambo baada ya kulisikia na kuafikana nalo pasipo mashaka yoyote akijiridhisha juu ya hayo ndipo atakapo jenga imani yake juu ya hilo jambo, katika Ukristo watu humpokea na kumuamini Bwana Yesu Kristo kupitia Neno lake ambalo ndiye yeye Mwenyewe ,katika kuhubiriwa kwa Neno juu ya Kristo atakayesikia na kuamini katika hilo neno la uzima pasipo na wasiwasi wowote basi atampokea Yesu Kristo na kuokolewa bali asiye amini atahukumiwa.
Marko 16:15-16
Akawaambia, enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka asiye amini, atahukumiwa.
Mpaka hapo tumeona katika kuamini juu ya Neno (Yesu Kristo), kuna pande mbili kuokolewa au kuhukumiwa, na naamini kabisa hakuna mtu yeyote anayependa kuhukumiwa juu ya kutokuamini Bali wote tunapenda kuokolewa lakini ushindani uliopo kati ya Roho na mwili ndivyo vinaleta kuangua katika kuto kuamini kwa walio wengi.
Yohana 3:14-18
Na kama vile Musa, alivyomwinua yule nyoka jangwani vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa. Ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee Bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulwenguni ili auhukumu ulimwengu, Bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye haukumiwi, asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwasababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.
Katika andiko hili la Yohana 3:14-14 ,tumeona tena dhahiri juu ya kutokuamini juu ya ujio wa Bwana Yesu Kristo katika mwili, kuwa Ni kuhukumiwa.
Na pia katika Marko 16:15-16, tumeona yakuwa atakaye amini na kubatizwa ataokoka.
Katika utaratibu wa makanisa mengi duniani watu wamekuwa wakijitambulisha kwa namna ambayo itawafanya wengine wawaone kuwa wameokoka na kumpokea Yesu kwa maneno ya vinywa vyao mfano: naitwa Fulani fulani, nimetokea mkoa wa Kilimanjaro, kanisa la Mahali fulani nimeokoka na nnapenda Yesu. Ni jambo jema kutamka wazi juu ya hilo lakini kama maisha yako halisi hayaliishi neno itakuwa sauti ulitoitoa mbele ya watu mahali hapo ni bure kabisa,
Wokovu halisi ni kumfanya Yesu kristo kuwa Bwana na Mwokozi wako, tukizungumza juu ya Bwana, yaani kumfanya Yesu Kristo kuwa Bwana wako, ni kwamba kila jambo utakalo lifanya katika maisha yako ni lazima liwe sawa na jinsi Yeye alivyosema katika Neno lake, kwa maana Biblia takatifu imeelezea juu ya mwenendo mzima wa Mkristo halisi, Yesu Kristo ni Neno sasa ikawa unasema umeokoka alafu hufuati jinsi vile Neno linavyosema katika Biblia Takatifu hakika wewe utakuwa ni muongo na mpingaji wa Neno yaani mpinga Kristo kwasababu mwanadamu anaweza kujichagulia Yale yaliyo rahisi kufanya kwake na kuacha
Kufanya Yale ambayo anaona kuwa yatamnyima uhuru, na pia anaona labda yamepitwa na wakati kwasababu ya kukua kwa utandawazi duniani, na mtu huyo yupo tayari kujiita mkristo wa kisasa kwasababu yeye anaenenda kama Jinsi ulimwengu unavyoenda na anajaribu kukiri kuwa ameokoka sasa mtu kama huyo tayari amekwisha potea katika lile shimo la uharibifu hebu tutazame haya maandiko kidogo,
Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele.
Vyema, Sasa kama Maandiko yameeleza juu ya kutokubadilika kwa Yesu Kristo (Ambae ni Neno) kwa kuzungumzia juu ya sheria alizozisema na kuagiza zitendeke kwa wale watakao mkubali na kumpokea na kuzifuata njia zake iweje Leo mtu ajiite mkristo wa kisasa? Huyo tayari atakuwa ni miongoni mwa wale makristo wa uongo walioelezewa katika kitabu cha Mathayo 24:24 ,Kwa kuwa Yesu Kristo (Neno) habadiki na wale tutakao kubali kumfuata haitupasi kubadilika kutokana na mvutano wa ulimwengu na imani yetu juu ya Yesu Kristo, inatupasa kuishi katika ule msimamo ambao Biblia Takatifu imeelezea juu ya Mkristo halisi sasa na kipimo halisi cha Mkristo aliye okoka sio ukali wa sauti yake, sio namna ambayo anaombea watu na kutoa pepo, sio kwasababu ya kuona maono na kutabiri, sio kwa kujifanya kutoa sauti ya chini sana, wala sio kwa upendo wa kinafiki(upendo bandia), sio kwa kuanzisha mapambio mazuri ya kuabudu, sio kwa kunena kwa lugha kama watu wengi walivyo potoka, Bali Mkristo halisi utamjua kupitia maisha yake halisi ule uhalisia ambao Mkristo anaishi ndio jambo pekee litakalokufanya uwe umekamilika ndani ya Kristo ,maana kwa vigezo nilivyoorodhesha hapo juu shetani pia huvitumia tu vizuri kwa watu wake humo makanisani maana waweza kuona mtu ana nena kwa lugha, anaimba vizuri, au anaomba kwa ukali wa sauti lakini kumbe katika uhalisia wa maisha yake unakuta ni mzinzi, mlevi, mtu wa kutumia lugha chafu ya matusi maana sio katika kuliita jina la Bwana ndio itaonyesha umeokoka kwasabu ipo siku ya kukanwa huku ukijitetea kuhusu kulitumia jina la Bwana, tusome tena haya maandiko hapa kidogo,
21. Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22.Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23.Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Tuutazame msatri wa 21, unavyoeleza ,unadhihirisha kwamba si kila mtu amuambiaye Bwana, Bwana ataingia mbingini Bali yule atimizaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni akimaanisha wale watakao enenda katika zile njia ambazo Bwana wetu Yesu Kristo alizileta ulwenguni ili watu waenende katika hizo ili kumtukuza Yeye kama vile kazi yake ya kushuka duniani alivyoitiliza yeye mwenyewe.
Tutazame Mstari wa 22, unavyoelezea, unadhihirisha ya kwamba wapo watu duniani wanatumia Jina la Bwana Yesu Kristo kutoa pepo, kutabiri, kufanya miujiza mingi lakini wameshindwa kutimiliza ule ushuhuda wa maisha yao halisi katika Kristo ndio maana mwisho wa mstari wa 22 kuna alama ya kuuliza yani wale watu sasa wanajitetea katika lile jina wakidhani ya kuwa kwa kulitaja taja tuu bila ule ushuhuda halisi wa maisha yao ni bure .
Tuutazame mstari wa 23, sasa hapa ndo panaonyesha jinsi wale waliojifanya kutumia Jina la Bwana Yesu kristo na wakashindwa kutimiliza ushuhuda wa Neno katika maisha yao wanavykataliwa na Bwana Yesu mwenyewe kwa Kuwait's waovu, ndugu ukishindwa kuliishi neno na maisha yako kufanyika ushuhuda juu ya Kristo Yesu lazima utakuwa mtenda maovu na sababu kuu iliyo mfanya Yesu Kristo awakatae ni kule kuwa katika Milki nyingine ya muovu ibilisi ,ukishimdwa kuishi ushuhuda wa Neno katika maisha yako ibilisi atakutumia vizuri sana.
Kabla hujatamka mbele za watu juu ya wokovu wako hakikisha unaliishi Neno ipasavyo maana ukishimdwa kuishi ushuhuda wa Neno katika Maisha halisi Bila shaka utakuwa upo upande wa pili wa kutenda maovu na kwa lugha nyepesi utakuwa unatumia wokovu kuficha yaliyo mabaya katika maisha yako halisi.
11 Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.
12 Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.
Kufanya Yale ambayo anaona kuwa yatamnyima uhuru, na pia anaona labda yamepitwa na wakati kwasababu ya kukua kwa utandawazi duniani, na mtu huyo yupo tayari kujiita mkristo wa kisasa kwasababu yeye anaenenda kama Jinsi ulimwengu unavyoenda na anajaribu kukiri kuwa ameokoka sasa mtu kama huyo tayari amekwisha potea katika lile shimo la uharibifu hebu tutazame haya maandiko kidogo,
Waebrania 13:8
Vyema, Sasa kama Maandiko yameeleza juu ya kutokubadilika kwa Yesu Kristo (Ambae ni Neno) kwa kuzungumzia juu ya sheria alizozisema na kuagiza zitendeke kwa wale watakao mkubali na kumpokea na kuzifuata njia zake iweje Leo mtu ajiite mkristo wa kisasa? Huyo tayari atakuwa ni miongoni mwa wale makristo wa uongo walioelezewa katika kitabu cha Mathayo 24:24 ,Kwa kuwa Yesu Kristo (Neno) habadiki na wale tutakao kubali kumfuata haitupasi kubadilika kutokana na mvutano wa ulimwengu na imani yetu juu ya Yesu Kristo, inatupasa kuishi katika ule msimamo ambao Biblia Takatifu imeelezea juu ya Mkristo halisi sasa na kipimo halisi cha Mkristo aliye okoka sio ukali wa sauti yake, sio namna ambayo anaombea watu na kutoa pepo, sio kwasababu ya kuona maono na kutabiri, sio kwa kujifanya kutoa sauti ya chini sana, wala sio kwa upendo wa kinafiki(upendo bandia), sio kwa kuanzisha mapambio mazuri ya kuabudu, sio kwa kunena kwa lugha kama watu wengi walivyo potoka, Bali Mkristo halisi utamjua kupitia maisha yake halisi ule uhalisia ambao Mkristo anaishi ndio jambo pekee litakalokufanya uwe umekamilika ndani ya Kristo ,maana kwa vigezo nilivyoorodhesha hapo juu shetani pia huvitumia tu vizuri kwa watu wake humo makanisani maana waweza kuona mtu ana nena kwa lugha, anaimba vizuri, au anaomba kwa ukali wa sauti lakini kumbe katika uhalisia wa maisha yake unakuta ni mzinzi, mlevi, mtu wa kutumia lugha chafu ya matusi maana sio katika kuliita jina la Bwana ndio itaonyesha umeokoka kwasabu ipo siku ya kukanwa huku ukijitetea kuhusu kulitumia jina la Bwana, tusome tena haya maandiko hapa kidogo,
Mathayo 7:21-23
22.Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23.Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Tuutazame msatri wa 21, unavyoeleza ,unadhihirisha kwamba si kila mtu amuambiaye Bwana, Bwana ataingia mbingini Bali yule atimizaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni akimaanisha wale watakao enenda katika zile njia ambazo Bwana wetu Yesu Kristo alizileta ulwenguni ili watu waenende katika hizo ili kumtukuza Yeye kama vile kazi yake ya kushuka duniani alivyoitiliza yeye mwenyewe.
Tutazame Mstari wa 22, unavyoelezea, unadhihirisha ya kwamba wapo watu duniani wanatumia Jina la Bwana Yesu Kristo kutoa pepo, kutabiri, kufanya miujiza mingi lakini wameshindwa kutimiliza ule ushuhuda wa maisha yao halisi katika Kristo ndio maana mwisho wa mstari wa 22 kuna alama ya kuuliza yani wale watu sasa wanajitetea katika lile jina wakidhani ya kuwa kwa kulitaja taja tuu bila ule ushuhuda halisi wa maisha yao ni bure .
Tuutazame mstari wa 23, sasa hapa ndo panaonyesha jinsi wale waliojifanya kutumia Jina la Bwana Yesu kristo na wakashindwa kutimiliza ushuhuda wa Neno katika maisha yao wanavykataliwa na Bwana Yesu mwenyewe kwa Kuwait's waovu, ndugu ukishindwa kuliishi neno na maisha yako kufanyika ushuhuda juu ya Kristo Yesu lazima utakuwa mtenda maovu na sababu kuu iliyo mfanya Yesu Kristo awakatae ni kule kuwa katika Milki nyingine ya muovu ibilisi ,ukishimdwa kuishi ushuhuda wa Neno katika maisha yako ibilisi atakutumia vizuri sana.
Kabla hujatamka mbele za watu juu ya wokovu wako hakikisha unaliishi Neno ipasavyo maana ukishimdwa kuishi ushuhuda wa Neno katika Maisha halisi Bila shaka utakuwa upo upande wa pili wa kutenda maovu na kwa lugha nyepesi utakuwa unatumia wokovu kuficha yaliyo mabaya katika maisha yako halisi.
1 Petro 2:11
12 Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.
Bwana Yesu Kristo akubariki
Comments
Post a Comment