Skip to main content

KANISA LA MUNGU WA KWELI ALIYE HAI, NA NGUZO YA MSINGI WA KWELI

Biblia Takatifu kamwe haijawahi kukosea katika kutuelekeza njia sahihi ya kuishi na kuenenda katika ibada zetu kama Wakristo halisi, yapo Makanisa mengi sana duniani tena katika nyakati hizi za mwisho na mengine yalikuwako tokea miaka Mingi sana iliyopita, naYanaenenda katika njia tofauti tofauti, hili likimpinga yule, lingine likijaribu kujiinua juu ya lingine lakini yote hayo ni yamesababishwa na kanuni za imani zilizo wekwa ndani ya Makanisa hayo yaani Madhehebu , maana katika Madhehebu zipo kanuni ambazo zinakuwepo kuendesha dhehebu husika , na pia kanuni za imani juu ya dhehebu moja na jingine huwa zinatofautiana sasa tujiulize Kama wote tunanajiita wakristo na tunamuamini Bwana Yesu Kristo kuwa ndiye Neno iweje Leo watofautiane katika hilo Neno? tuangalie mfano halisi dhehebu la Lutheran wanabatiza watoto wadogo, na wanaruhusu wanawake kuhubiri,ukiangalia Roman catholic pia wanabatiza watoto wadogo lakini hawarusu wanawake kuhubiri , Pentekoste nao wanabatiza watu wazima kwa maji Mengi ila wana wahubiri wanawake, vivyo hivyo kwa wa Paptisti, Methodist na wengineo wrote hap kanuni za imani hazifanani yaani zinapimgana, sasa kama kweli tunafuata Neno kiuhalisia je? Utofauti  huo kati ya wanaojiita Wakristo ungetokea? Iweje mkristo uwe Mkristo alafu Mpaptisti au Methodist? Lazima kutakuwa na imani tofauti zimejijenga ndani ya hao wanao jiita wa dhehebu Fulani kama Biblia Takatifu limesema imani ni moja ,na Ubatizo mmoja iweje Leo kila dhehebu Lina namna yake ya kubatiza? Huoni huko ni kutoka nnje ya Neno??
Tusome,  

 Waefeso 4:5 

Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.
Kama Bwana ni mmoja ,imani moja na ubatizo mmoja iweje Leo kuwe na tofauti kati ya mambo haya ? Huoni kuwa huo sio mpango wa Mungu kuwa na imani zinazoleta tofauti katika Ukristo halisi.
Hivyo ndiyo kweli ya Mungu neno lake ndilo kweli sasa watu wamejiaminisha katika kanuni hizo za imani  (Madhehebu) kuona ya kuwa ndipo mahali salama kumbe sio, haukuwa mpango wa Mungu kuwepo kwa Kanuni zinazoongoza kanisa kinyume na zile zilizo agizwa kwenye Neno kupitia Mitume wake,  watu hujua ya kwamba mahali anapoona anapata sana ,utajiri wake umekuwa sana anaona ndipo mahali lake lakini katika Neno ni pale nafsi yako itakapo tulia bila kuwa na shaka lolote juu ya kinachotendeka kanisani na jinsi Neno Linavyosema maana muongozo wa mwenendo wa Kweli WA kanisa la Mungu aliye hai upo katika Biblia, na watu wameikataa ile KWELI lile Neno la muongozo wa Kanisa la KWELI na kuenenda katika njia zao wanazoona zinafaa na zina maslahi kimwili wala si kiroho, kwa kuwa Biblia haijawahi kuacha maneno juu juu huwa inaelezea wazi juu ya wale wanaoikataa KWELI na kuenenda katika njia zao ambazo ndizo hizo zimeleta kanuni za imani,
Tusome Maandiko,

 2 Wathesalonike 2:13

10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
11 Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo;
12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.
13 Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli;
Kweli inayo zungumziwa hapo ni Neno na Neno ndiye Kristo Yesu, sasa zile kanuni zote za Ki Biblia juu ya mwenendo wa kanisa zipo ndani ya Neno sasa ukilikataa Neno, ambalo ndilo  KWELI Mungu ataachilia nguvu ya upotevu uzidi kuuamini huo uongo, sasa tuone kwenye hizo kanuni za imani watu wamekuwa wakiziamini pasipo kuzipima kaitika Maandiko matokeo Yake wanakuja kuingia katika hukumu ya kuikataa KWELI pasipo kujua, na nguvu ya upotevu   ikisha achiliwa utaendelea kujiona kuwa upo sahihi na unafurahia vile unavyovipata kumbe ni furaha ya udhalimu, ndugu msomaji usiamini kanuni yeyote ya imani pasipo kuipima katika Neno, maana ibilisi ni mwerevu sana hupita katika vitu vidogo na kukuangusha katika sehemu kubwa (anguko kuu). Kuijua KWELI na kuiamini na kubaki katika KWELI yaani Neno sio jambo dogo linahitaji maombi na kusimama kweli kweli pasipo kuyumbishwa na dunia pamoja na mambo yake, yamkini waweza kuwa umefungwa ndani ya hizo kanuni na unaona ugumu kuzikataa Fanya maombi juu ya njia sahihi na mahali pako kwa Jina la Bwana Yesu Kristo naye atakushindia na mitego ya Adui.
Maana yote hayo yanatokana na mapokeo tofauti tofauti ambayo yanaligeuza Neno, na kama jinsi Biblia Takatifu ilivyo eleza hayo ilikiwa ni yale mafundisho ya kwanza yaliyo kwisha kutolewa na mitume juu ya mwenendo wa kanisa na njia za Mkristo halisi ,mtu mwingine atakaye jaribu kuyabadilisha kwa kufundisha tofauti na ilivyo fundishwa mwanzoni na Mitume basi amelaaniwa tusome maandiko haya kidogo,

Wagalatia 1:8

 Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.
Aliye kuwa akiyanena hayo ni mtume Paulo kwa wagalatia, sasa hebu tuone kidogo juu ya Mtume Paulo ,
Wagalatia 1:1
Paulo, mtume, (si mtume wa wanadamu, wala kutumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu),
Umeona kitu hapo? Paulo hakutumwa na mwanadamu Bali ni Yesu Kristo Mwenyewe hivyo Yale Paulo alikuwa akifundisha ,akiwaelekeza watu namna ya kuenenda katika kanisa na mienendo ya Wakristo haikuwa ni Yeye Bali ni Yesu Kristo alyekuwa ndani yake akisema na watu wake, hivyo kwa Makanisa yaliyo jiwekea utaratibu wake yenyewe na kuaminisha waumini wao kuwa ni kweli na huku wameenenda kinyume na Yale ambayo Yesu Kristo aliagiza kupitia mitume wake juu ya mwenendo mzima wa kanisa , tayari ile laana i juu yao.
Sasa tuone mwenendo wa Kanisa la MUNGU aliye HAI ,na Msingi wa Kweli kama vile Bwana Yesu Kristo alivyo nena kupitia Mitume Paulo kwa watu wake, na tukumbuke kwenye Wagalatia 1:1 ,inavyoeleza kuwa Mtume Paulo hakutumwa na mwanadamu, ni Yesu Kristo alikuwa ndani Yake akinena.


1. WANAUME WASALISHE KILA KUTAKAPO KUWAKO NA IBADA:

1 Timotheo 2:7-8

7 Nami kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mhubiri na mtume, (nasema kweli, sisemi uongo), mwalimu wa Mataifa katika imani na kweli. :
8 Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano.
Mtume Paulo aliyanena haya kama vile Kristo Yesu alivyomuagiza, na kwa historia,  ya miaka ya nyuma sana katika Makanisa wanaume walikiwa wakisalisha maana walilijua hilo kiwa ni agizo kutoka kwa Mungu, na Madhehebu mengi yalikuwa yakifanya hivyo lakini eti kutokana na utandawazi  na kwenda na wakati  sasa dunia imebadilika wamejifanya kusahau hilo na kurususu wanawake kusalisha kwenye ibada, sasa hapo tunaona ya kuwa kanisa limebadilishwa na wakati, yamkini mda unavyozidi kwenda watoto wataanza nao kusalisha makanisani sasa kwa jambo hilo la kugeuza wanawake kusalisha badala ya wanaume ni kuenenda kinyume na Neno na hilo kanisa sio tena kanisa la Mungu aliye HAI, na msingi wa kweli, Bali limekwisha potea katika waabudio halisi.

2. MA ASKOFU, WACHUNGAJI NA MASHEMASI WAWE WAUME WA MKE MMOJA:

1 Timotheo 3:1-12

1 Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema.
2 Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha;
3 si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha;
4 mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu
5 (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?)
8 Vivyo hivyo mashemasi na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana,si watu wanaotamani fedha ya aibu.
9 wakiishika siri ya imani katika dhamiri safi.
10 Hawa pia na wajaribiwe kwanza; baadaye waitende kazi ya shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia.

11 Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote.

12 Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao.
13 Kwa maana watendao vema kazi ya shemasi hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu.

Kwa kuwa kanisa huundwa na sehemu nyingi za uwajibikaji, ikiwemo wafundishaji na wahudumu wa kanisa katika shuhuli mbali mbali zitakazo fanyika kanisani au wakati wa ibada, tukiwa tumefikia katika nyakati za haki sawa kwa wote watu wamesahau Neno NA kufuata ulimwengu na kusoma kama wachungaji wanatakiwa wawe wanaume tu au mashemasi wawe wanaume tu wakaona haki itendeke kwa wrote wanawake nao wahubiri na pia nao tena wawe mashemasi umeona? Shetani jinsi alivyo mwerevu? Amejaribu kuharibu taratibu za kanisa ili mile kitakacho tendeka kanisanj kisiwe na kibali mbele za Mungu, angalia ulimwengu wa sasa jinsi Makanisa mengi yalivyo na wahubiri wanawake na mashemasi wanawake kitu ambacho ni kinyume na Neno, hizo ni taratibu za Kibinadamu katika kanisa wala si kwa kufuata Biblia Takatifu.

3. WANAWAKE HAWARUHUSIWI KUSALISHA NA KUHUBIRI INJILI 
 1 Timotheo 2:8
Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano.

Katika kanisa la MUNGU WA kweli aliye hai na Msingi wa kweli mwanamke haruhusiwi kusalisha kabisa maana kanisa la Kweli huongozwa kwa misingi ya Neno yaani Bwana YESU kristo mwenyewe na sio kwa kuangalia mabadiliko ya Ki ulimwengu maana Neno halibadiliki kamwe, Tukizungumzia kusalisha tunahusisha matukio yote ambayo hufanyika ili kuwaweka watu tayari kupokea Neno au kuwaongoza katika jambo litakalo hitajika kufanyika popote kunapokuwako na uhitaji wa injili kuhubiriwa, kwa wakati husika mambo kama hayo ni kuongoza ibada na kuongoza sifa (yaani kuanzisha nyimbo), hivyo basi kama kanisa litaongozwa kwa misingi ya Neno utaratibu huo utafuatwa lakini kama litaendeshwa kama vile dunia inavyobadilika (utandawazi) kwa kudai haki sawa hadi kanisani wanawake watachukua hizo nafasi na hilo kanisa halitakuwa la MUNGU aliye hai na msingi wa kweli.


1 Timotheo 2:11-14

11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.
12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.
13 Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye.
14 Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.
Katika kanisa la Mungu aliye HAI tena msingi wa kweli mwanamke haruhusiwi kuhubiri, Bali amepewe kusikiliza katika utulivu, lakini siku hizo wanawake wahubiri wapo wengi kweli katika madhehebu mengi na pia hata Yale yanayo jiita makanisa pasipo kujua maana yake, sasa yote hii imetokana na watu kupata ujasiri wa kulipinga Neno, na kulipinga Neno maana Neno ni Bwana YESU Kristo sasa itakuaje mpinga Kristo anahubiri habari za Neno huku nalipinga Neno?
Na watu wamepotoshwa na kuamini juu ya wahubiri wanawake wengine hata wakidiriki kuwasifia kwamba muhubiri Fulani mwanamke anaupako kumbe tauari wrote mmekwisha poyea katika kuuamini uongo na kuikataa kweli, hivyo kuwepo kwa miujiza au ishara anazozifany huyo mhubiri wa mwanamke sio kipimo cha kuwa yeye ni wa kweli, Bali kinachompima kuwa yeye anafuata usahihi ni kumpima kwenye Neno. Hivyo watuu wache kufuata wanachokiona Bali wakipime katika Neno na ndipo wakiamini.

BWANA YESU KRISTO AKUBARIKI

UJUMBE WA NYAKATI KWA UFUNUO WA BWANA YESU KRISTO KATIKA KUMUANDAA BIBI HARUSI WAKE KUPITIA MJUMBE WAKE BRO. WILLIAM MARION BRANHAM.

Comments

Popular posts from this blog

NJIA YA KWELI YA WOKOVU KULINGANA NA BIBLIA

Ikiwa ipo njia ya kweli ya wokovu, bila shaka na kwa uhakika njia ya uongo nayo itakuwepo maana Neno ambalo limeandikwa kwenye Biblia takatifu limeonyesha juu ya uongo na ukweli,  na kuwepo kwa roho ya uongo juu ya Ukristo halisi:,       1 Yohana 4:1-6   Wapenzi , msiamini kila roho kwamba zimetokana na Mungu Bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwasababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu na hii ndiyo Roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani. Ninyi watoto wadogo, mnatokana na Mungu ninyi mmewashinda, kwasababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia. Hao ni wa dunia; kwahiyo hunena ya dunia na dunia huwasikia; Sisi twatokana na Mungu yeye amjuaye Mungu atusikia; Yeye asiyetokana na Mungu hatusikii. Katika hili ...